Comments


ANG'ATWA UUME NA NYOKA AINA YA CHATU

Raia mmoja wa Thailand anaendelea kuuuguza
jeraha katika hospitali moja baada ya nyoka aina
ya chatu kutokea ndani ya choo na kumng’ata
uume wake. Attaporn Boonmakchuay, ambaye
alipoteza damu nyingi amesema kuwa nyoka
hiyo ilikuwa ikimvuta baada ya yeye na mkewe
kujaribu kuipiga.
Madaktari wanasema kuwa Bw Attaporn ambaye
alipoteza damu nyingi anaendelea vyema na
matibabu. Wafanyikazi walilazimka kukiharibu
choo hicho.Baadaye nyoka huyo aliachiliwa na
kuingia msituni.
Kisa hucho kilitokea wakati ambapo Attaporn
mwenye umri wa miaka 38 alielekea katika choo
chake nyumbani kwake huko
Chachoengsao,mashariki mwa Bangkok kabla ya
kwenda kazini siku ya Jumatano. Wakati
alipokuwa akitumia choo hicho alihisi uchungu
mkali.
”Nilihisi kama ambaye uume wangu ulikuwa
umekatwa,Nyoka huyo alikuwa akinivuta kwa
kutumia nguvu nyingi”,alisema.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system