Comments


Maonyesho ya bidhaa za Plastiki , kufikia tamati kesho Mei 29



Maonyesho ya bidhaa z Plastiki yaliyoanza jana Mei 27.2016  katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam yanatarajia kufikia tamati hiyo kesho Jumapili ya Mei 29.

Maonyesho hayo  ambayo Tanzania ni mwenyeji  kwanza  ya bidhaa za plastiki, mpira, kemikali za petrol na ujenzi  yanakuwa ya kipekee huku watu mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijiniDare s Salaam.

Awali Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat ambao ni waandaaji wa maonyesho hayo,  alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zinashiriki katika maonesho hayo.

Afrika –PPB-EXPRO   ni  jukwaa la kipekee la bidhaa mpya  na yatatoa mwanya wa kuyaelewa  masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.

 “Maonesho haya yamebuniwa kwa lengo la  kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara  kati ya Misri na Tanzania na hali kadhalika  kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,kubainisha  kuwa Tanzania ni ya kwanza  katika orodha ya nchi za Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.

Alisema kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO  inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji  walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.

Barakat alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili kuweza  ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system