Comments


FARID MUSSA ATUA NCHINI AKITOKEA HISPANIA

Winga machachari wa klabu ya Azam FC, Farid Mussa, amewasili nchini na kusema yupo fiti kukabiliana na changamoto ya soka la Hispania endapo atajiunga na Club Deportivo Tenerife msimu ujao.

Farid ameiambia Goal alijitahidi kupambana na kufanya vizuri kwenye majaribio yake kwa lengo la kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na anafurahi kwa mapokezi mazuri na ushirikiano alioupata kwa siku zote alizokuwa huko.

“Nimekutana na hali ya hewa na mandhari tofauti na hapa, pia vyakula navyo ni tofauti sana hivyo ilinichukua muda kuzoea mambo yote hayo, hata mfumo wa uchezaji na mazoezi ya wenzetu ni tofauti sana, mwanzo ilinipa shida sana lakini hivi sasa nimezoea na kuona ni kawaida sana.

“Hata wenyewe walinishangaa sana kwa namna nilivyozoea haraka na nilivyokuwa nacheza, naweza kusema nipo fiti hivi sasa kupambana na changamoto zote kule,” alisema.

Winga huyo, 20, mwenye kasi kubwa uwanjani na msumbufu kwa wachezaji wa timu pinzani kwa chenga zake za maudhi, pia alichukua fursa hiyo kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kujaalia mafanikio kwenye safari yake hiyo.

Winga huyo wa Azam amerejea Dar es salaam baada ya kumaliza majaribio ambayo yalifanikiwa kwa kiwango kikubwa na anasubiri kujiunga na Teneriffe msimu ujao
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system