Comments


manyambizi wa njano wa angukia pua na kuifanya Liverpool kupaa Fainali.






Liverpool fansJurgen Klopp amefanikiwa kufikisha Liverpool kwenye hatua ya fainali ya Europa League kwenye msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo baada ya kuifunga Villarreal kwenye mchezo wa maruadiano wa nusu fainali.
Akipoteza kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ugenini, Liverpool walianza kupata matumaini kwenye mchezo wa jana usiku baada ya Bruno Soriano kujifunga na kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1.

Daniel Sturridge akamalizia kazi nzuri ya Roberto Firmino kisha Lalana akazamisha matumaini ya manyambizi wa njano kwa kupachika bao la tatu na kufanya matokeo kuwa 3-0 huku matokeo ya jumla (aggregate) yakiwa ni Liverpool 3-1Villarreal.

Liverpool itakutana na Sevilla ambayo usiku wa jana ilipata ushindi wa magoli 3–1 dhidi ya Shakhtar Donetsk wakati mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya kufungana magoli 2-2. Kwahiyo matokeo ya jumla ni Sevilla 5-3 Shakhtar Donetsk.

Tuitazame historia kwa ufupi
Liverpool ilishindwa kufunga goli kwenye mchezo mmoja kati ya michezo 21 ya Europa League (Liverpool 0-0 Braga mwezi December 2010)
Daniel Sturridge amefunga kwenye mechi nne kati ya tano zilizopita alizocheza kwenye uwanja wa Anfield kwenye mashindano yote.
James Milner ndiye mchezaji mwenye assists nyingi (14) ndani ya Liverpool msimu huu akifuatiwa na Roberto Firmino (9)
Majogoo wa jiji watakutana na wapinzani kutoka Hispania kwenye mchezo wa fainali ya mashindano ya Ulaya kwa mara ya tatu, wakiwa wameshacheza dhidi ya Real Madrid mwaka 1981 kwenye European Cup Final (walishinda 1-0) na Alaves mwaka 2001 kwenye UEFA cup (walishinda 5-4 baada ya dakika za nyongeza)
Villarreal wamepoteza michezo yao minne ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system