Comments


MTOTO WA MIAKA MINNE ATEKETEA KWA MOTO MWANZA.

MTOTO Vestina Masolwa (4) wa kitongoji cha
Nyamungu– Mwabagole katika kata ya
Mwangalangha tarafa ya Ndugu wilaya ya
Kwimba mkoani Mwanza, amefariki dunia baada
ya kuteketea kwa moto jikoni wakati nyumba
yao ikiteketea kwa moto.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 9 alasiri katika
kitongoji hicho, baada ya mama wa marehemu,
Grace Wilson (30), kupika chakula na kisha
kwenda shambani nje kidogo na nyumba hiyo
akiwa amemuacha mtoto huyo jikoni.
Kwa mujibu ya taarifa ya Kamanda wa polisi
mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema
baada ya mama huyo kwenda shambani na
kumuacha mtoto wake (marehemu), alianza
kuchezea moto uliosababisha nyumba yao
kuungua.
“Wakati mama wa marehemu akiwa anaendelea na
shughuli zake shambani, aliona nyumba yake
ikiungua moto na kuamua kukimbia kurudi
nyumbani na kukuta nyumba ikiteketea na
kusababisha mtoto Masolwa kufariki dunia papo
hapo."
Kamanda Msangi alisema mwili wa marehemu
tayari ulifanyiwa uchunguzi na daktari kisha
kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili
ya mazishi, lakini chanzo cha tukio hilo likidaiwa
ni uzembe wa wazazi kushindwa kuwa
waangalifu kwa mtoto huyo na kusababisha kifo
na nyumba kuungua.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wazazi wawe makini
na waangalifu wakati wote na watoto ili
kuwaepusha na ajali zinazoweza kuepukika,
huku pia akiwataka kuhakikisha kabla
hawajaondoka kwenda kwenye shughuli zao za
kila siku, wanawaacha watoto wao kwenye
mazingira salama.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system