Comments


WEMBE NI ULE ULE VANGAL KUONDOKA> LICHA YA UNITED KUTWAA KOMBE LA FA


Licha ya kuiwezesha Manchester United kushinda Kombe la FA jana Jumamosi lakini hilo halijazuia Man United kuachana na kocha wake, Louis Van Gaal ambaye ameshindwa kuisaidia klabu hiyo kuingia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA kwa msimu ujao.

MItandao mbalimbali ya habari za michezo ikiwemo Skysports na ESPN imeripoti kuwa kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho ndiyo kocha mpya wa Manchester United na kinachosubiriwa kwa sasa ni kumtangaza kocha huyo ambaye ataanza kuinoa Man United msimu ujao.

Mitandao hiyo imeripoti kuwa awali Van Gaal alikuwa bado hajapatiwa taarifa kuwa nafasi yake itachukuliwa na Mourinho kutokana na kocha huyo kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Man United na alipatiwa taarifa ya Mourinho kuchukua nafasi yake siku ya Jumatano.

Jana baada ya Manchester United kushinda Kombe la FA wakati akizungumza na waandishi wa habari, Van Gaal alikataa kuzungumza kuhusu hatma yake ndani ya Manchester United kama bado atakuwepo au ataondoka.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system