Ujio wa Kocha Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United kunaweza kuwa sababu mojawapo ya kumbakiza kipa wa Man United, David De Gea ambaye kabla ya kuchukuliwa kwa Kocha Mourinho alinukuliwa akisema kama Van Gaal atasalia klabuni hapobasi yeye ataondoka.
Akizungumza la gazeti la Marca la Hispania, De Gea almtaja Mourinho kama moja ya makocha bora na anataraji kushinda mataji kwa misimu inayofuatia.
“Kuzungumza kuhusu Jose ourinho ni kuzungumza kuhusu kocha anaye shinda, na huo ndiyo utamaduni wa Manchester United na hata kwangu. Kwa mtazamo wangu tutakuwa na timu kubwa. Ninamkaribisha,” alisema Mourinho.
0 comments:
Post a Comment