Comments


Waziri Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye; Ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Ya CHADEMA

Waziri Mkuu Mstaafu,Fredrick Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mwenyekiti wa Chadema – Taifa Freeman Mbowe,amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.

Amesema, dhamira ya Chadema ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.

Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteuwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system