Msomaji wa makala ya ndoano hii leo nimeweza kukuchambuli tu kwa uchache kuhusiana na samaki aina ya Nguva,yafahamu mengi yaliyomo ndani ya NGUVA.
.UKWELI KUHUSU SAMAKI AINA YA NGUVA JE NI
KWELI SAMAKI MTU ?
.JE WAJUA KUWA NYAMA YA NGUVA (SAMAKI
MTU}NI TAMU ZAIDI KULIKO YA NGOMBE.;
Nguva (Kisayansi: Sirenia) ni mnyama mwenye vikono vya mbele na mkia wenye
umbo la pembetatu anayeishi Bahari ya Hindi, Bahari
ya Karibi, Afrika ya Magharibi na mto wa Amazoni. Neno "nguva" pia ina maana ya mtu mwenye mwili wa
mwanamke na mkia wa samaki kama sireni wa mitholojia ya Kigiriki. Hula manyasi za bahari na mimea ya maji
mingine.
Nguva: Mnyama aelezwaye ndivyo sivyo
Watu wengi hawajui uhalisi wa
mnyama huYo kwani baadhi ya watu wamekuwa wakisema ni upande mmoja samaki na
mwingine mwanamke.
Bi REBECA MASAWE ambaye ni mwananchi wa
kawaida katika kulizungumzia hili alisema samaki hawa sio wa kawaida , yaani ni viumbe wa tofauti
sana kwa sababu wananyonyesha alafu ni samaki hatari sana.
" kwa hiyo mimi kwangu nawaita majini ya baharini sababu
kwanza hawapatikani pengine zaidi ya baharini, na maisha wanayoyaishi ni sawa
na binadamu sembuse tu wao wapo baharini. "
Alisema samaki huyo aina ya NGUVA bado wana nywele kama binadamu hivyo hivyo hawapendi hata kidogo,na hata akipatiwa samaki huyo hali.
Makumbusho ya taifa ambayo ndiyo
ina dhamana ya kuhifadhi mambo ya kale imeweka wazi ukweli kuhusu nguva na
maisha yake. Mkurugenzi wa Makumbusho hayo, Bw. Paul Msemwa, anasema
mnyama huyo mambo mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu mnyama huyo si ya
kweli.
Anasema nguva ni mnyama anayezaa
na kunyonyesha kama walivyo wanyama wengine. Anasema wakati akinyonyesha
husimama na kukumbatia mtoto wake hali inayoweza kumfanya mtu aliyemuona
kudhani kuwa ni mtu.
Anaeleza kuwa watu wengi hawajui
ukweli kuhusu nguva na baadhi wamekuwa wakisema kuwa ni nusu mtu. ``Kuna
watu wanapotosha wanasema nguva ni nusu mtu kwa maana kuwa chini ni samaki na
juu ni mtu lakini si kweli,`` anasema.
Anasema muda mrefu mnyama huyo
hukaa baharini na kwamba anapenda mazingira mazuri na tulivu. Dk. Msemwa
anasema mnyama huyo huzaa kila baada ya miaka mitatu au saba na huzaa mtoto
mmoja pekee. Mtoto wa mnyama huyo anapozaliwa huwa na kati ya kilo 153
hadi 200, wakati nguva mkubwa huwa na kati ya kilo 400 hadi 1, 000. Dk.
Msemwa anataja maeneo ambayo wanyama hao hupatikana kuwa ni Somanga karibu na
Rufiji, Kilwa, Mafia, Moa Mombasa, Tanga na Bagamoyo.
Anasema endapo mazingira ya
bahari yataendelea kuchafuka kuna uwezekano wa kiumbe hicho
kutoweka. Alisema kwa kawaida nguva hupenda maeneo tulivu na yasiyo na
vitisho.
``Huu uvuvi haramu wa mabomu na
baruti utasababisha wanyama hawa kutoweka kabisa kama jitihada za makusudi
hazitachukuliwa,`` Anasema mnyama huyo hupendelea zaidi kula majani yaliyo
chini ya bahari maarufu kama mwani.
Nguva ana rangi ya kijivu na umbo
la mwili wake ni nyofu na uso wa umbo la nguruwe.
Awapo katika maji hutoa kichwa
chake juu ya maji kuvuta hewa kwa kutumia mashimo mawili ya pua yaliyopo upande
wa juu wa kichwa chake.
Dk. Msemwa anasema nguva jike ana
chuchu kifuani na anaponyonyesha mwanaye husimama kwa kutumia mkia wake chini
na kumkumbatia mwanaye kama binadamu.
Aidha, anasema tayari wameanza
kuwaelimisha wavuvi kuhusu mnyama huyo ili wamwonapo wasimvue.
Pia amesema kuna wakati wavuvi
walikuwa wakiwavua na kuwala kwa kuwa nyama yao ni tamu zaidi ya ile ya ngombe.
kutokana na mazingira kuharibiwa, hivi sasa
mnyama huyo ameanza kutoweka sehemu ambazo alikuwa akionekana.
``Alikuwa akionekana Dar es
Salaam, Kimbiji, Buyuni, lakini sasa haonekani tena na hali hii inatokana na
usumbufu wa wavuvi na mazingira ya bahari kuchafuliwa,`` anasema.
mnyama huyo ana aibu na
anapogundua kuwa maeneo alipo kuna binadamu huhama na kwenda mbali zaidi. Dk.
Msemwa anasema vifo vya nguva vimekuwa vikitokana na ajali za bahati mbaya
mfano kunaswa kwenye vyombo vya kuvulia kama vile jarife, mishipi na kuongezeka
kwa shughuli za uvuvi.
Kwa upande wake, Mhifadhi mwandamizi ,Bi Adelaide Sallema alisema wameanza kuelimisha wavuvi ili
wanapowaona wanyama hao wasiwavue,Kwani kuna umuhimu wa kuweka maeneo tengefu
kwa ajili ya kuwahifadhi wanyama hao.
``Tumeishauri serikali itenge
maeneo ambayo mnyama huyo anapatikana ili wasitoweke,``
Amefafanua kuwa mtawanyiko wa
nguva upo zaidi maeneo ya Somanga, Kilwa, delta ya Rufiji, Mohoro na Mafia
kuanzia miaka ya 1960.
Amesema nguva amekuwa akionekana
mara nyingi zaidi miaka ya 1950 sehemu za Kilwa Kivinje miaka ya 1960 sehemu za
Mkwaja na Matapata miaka ya 1970 sehemu za Kilwa kisiwani, Kilwa Masoko na
kaole miaka ya 1980 sehemu za Somanga, Pombwe na Olelo miaka ya 1990 sehemu za
Masoko Pwani na miaka ya 2000 sehemu za Somanga, Utigi Ngolwe, Pombwe na
Mbonde.
Sehemu zingine zilizoripotiwa
kuwa na nguva ni Lamu, pangani, Tanga, Buyuni, Kimbiji, Unguja, Pemba, Mafia na
Kisiju. Dk. Msemwa anasema nguva anahitaji kuhifadhiwa kwa kutovuliwa kwa
manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho. Wakati huo huo, anasema ukumbi wa
kudumu wa viumbe (biolojia) ni kati ya kumbi nne za kudumu zilizopo Makumbusho
na Nyumba ya Utamaduni.
Alisema ukumbi huo ulianzishwa
rasmi mwaka 1980 baada ya kumbi nyingine kuwepo ambazo ni ukumbi wa chimbuko la
Mwanadamu, ukumbi wa historia ya Tanzania na ukumbi wa mila na desturi za
Mtanzania. Anasema ukumbi wa viumbe ulipoanzishwa ulilenga zaidi maonyesho
ya viumbe bahari na mara nyingi ulijulikana ukumbi wa viumbe bahari (Marine
Biology Gallery).
Ameainisha moja ya maonyesho yaliyopo katika ukumbi huo
ni maonyesho ya mnyama Nguva ambaye kwa mara nyingi amekuwa akiamisha maswali
na majibu ya aina mbalimbali kutoka katika jamii kama ni nusu samaki na nusu
mwanamke.
Anaeleza kuwa kutokana na
mahitaji mbalimbali ya jamii yaliyojitokeza, ilionekana kuwa ni sahihi kuwa na
viumbe kutoka katika mifumo ikolojia mbalimbali ili kuweza kukidhi
haja. Anasema kwa sasa mikusanyo iliyopo imegawanyika katika sehemu kuu
tatu kutokana na mifumo ikolojia ilikotoka mikusanyo hiyo.
Anatoa mfano wa mfumo ikolojia wa
bahari Wenye wanyama wanyonyeshao, samaki, kamba kochi, kasapweza, miamba
ya matumbawe, majongoo bahari, konokono na kaa.
Tuyatunze mazingira yetu hasa kwa
kuacha uvuvi haramu ambao umekuwa ndio chanzo kikubwa cha kutaka kuwapoteza
wanyama hawa,Kwani tukiyatunza tutakuwa
na nguva wengi na wataongeza sana kipata cha nchi kwani watalii kutoka katika
nchi tofauti tofauti tofauti watakuja kufanya utalii,
0 comments:
Post a Comment