Comments


VIROBA VYAPIGWA MARUFUKU

Mifuko ya plastiki inayofungasha pombe
maarufu kama ‘viroba’ imepigwa marufuku na
Serikali kuanzia mwakani.
Sambamba na hilo Serikali pia, imepiga
marufuku moja kwa moja utengenezaji,
usambazaji, uingizaji nchini wa mifuko ya
plastiki kuanzia mwaka huo.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira), January Makamba
aliwaambia wanahabari jana sehemu kubwa ya
mifuko hiyo inayotolewa bure imekuwa
ikichangia uchafuzi wa mazingira kwa kiasi
kikubwa.
Wakati Makamba akiyasema hayo, Februari
mwaka huu Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina
aliondoa zuio la matumizi ya mifuko ya plastiki
akisema kuwa itaziweka rehani ajira za
Watanzania wanaofanya kazi kwenye viwanda
vinavyotengeneza mifuko hiyo.
Pia, Mpina alisema itapunguza kasi ya uwekezaji
wa viwanda vilivyowekeza katika bidhaa hiyo.
Akizungumza katika siku ya Mazingira Afrika,
Mkurugenzi wa Mazingira, Dk Julius Ningu
alisema maamuzi hayo yamelenga kulinda
viwanda vilivyoajiri mamia ya Watanzania,
tofauti na nchi nyingine zinazotegemea
wazalishaji wa nje ya nchi.
Makamba akizungumzia uamuzi mpya wa kuzuia
mifuko ya plastiki, alisema matumizi ya mifuko
inayofungashia vileo na inayotumika katika
matumizi mengine husambaa na kuchafua
mazingira. Alisema mifuko ya plastiki inatajwa
kuziba mifereji na kusababisha mafuriko na
athari nyingine za mazingira.
“Leo (Jana), tumeamua kutangaza ili kuwaanda
wahusika wasiendelee kuwekeza katika mifuko hii
badala yake wasubiri utaratibu mwingine
utakaowekwa na Serikali,” alisema Makamba na
kuongeza kuwa:
“Asilimia kubwa ya uchafu kwenye nyanzo vya
maji, mito, maziwa na fukwe za bahari ni mifuko ya
plastiki.”
Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli,
alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya
ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu
dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja
mifuko hiyo.
Alifafanua kwamba Serikali itatoa muda kwa
walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye
biashara ya mifuko hiyo ili kujiandaa kuacha
shughuli hizo na badala yake itawezesha
mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa
vifungashio mbadala.
“Kwa wanaotengeza mifuko hii na kuiuza katika
soko la nje hatuna tatizo nao waendelee. Ila kwa
soko la ndani hawataruhusiwa kufanya hivyo.Zuio
hili litakuwa la kisheria siyo kwa
maneno,” alisisitiza Makamba.
Aliongeza kuwa katika kuonyesha Serikali
imedhamiria kupambana na hali hiyo wizara
yake imeamua kutuma timu ya watu watano
kwenda Rwanda kujifunza namna bora ya
kudhibiti matumizi na kuzuia mifuko hiyo tangu
mwaka 2008.
Waziri huyo alitoa wito kwa watengenezaji,
wasambazaji na waagizaji wa mifuko hiyo
kujiandaa na zuio hilo na katika siku zijazo
Serikali itatoa utaratibu na maelekezo ya tarehe
ya kuanza zuio huku taratibu nyingine za kina
zikifuata ili kuondoa mkanganyiko.
Katika hatua nyingine, Makamba alisema
maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Mazingira
Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka
hayatafanyika kitaifa badala yake wizara
imewaelekeza wakuu wa mikoa kufanya
maadhimisho katika maeneo yao.
“Tumewapa miongozo kuhusu utekezezaji wa
shughuli hizo za maadhimisho zinazolenga kutoa
hamasa ya hifadhi ya mazingira hususan nyanzo
ya maji amabayo ni muhimu kwa viumbe
hai,” alisema Makamba.
Kwa mujibu wa Makamba, kauli mbiu ya mwaka
huu kitaifa juu ya maadhimisho hayo ni ‘
tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa
letu’aliwashauri na kuwataka Watanzania
kutumia siku hiyo kupanda miti, kudhibiti
uchomaji wa misitu
Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold
Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki
nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi
jirani ya Kenya.
Alisema agizo la Waziri Makamba litawezekana,
lakini linahitaji ushirikiano kutoka kwenye sekta
zingine kwa kuwa viwanda vingi vya mifuko ya
plastiki vipo Kenya.
"NEMC tayari tulishaanza mazungumzo na
wazalishaji kuhusu mifuko ya plastiki,” alisema.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system