Comments


KIAFYA UNAJUA FAIDA ZA KUMSAMEHE MTU HIZI HAPA ZISOME

                    
















1. Hupunguza maumivu ya mwili, akili, na nafsi. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika katika chuo cha Duke kitengo cha madawa, kwa  watu 61 waliokuwa na maumivu makali ya mgogngo, ilibainika kuwa, watu wenye uwezo mkubwa wa kusamehe, hupunguza maumivu kwa asilimia 50!
2. Msamaha pia hupunguza tatizo la kukosa usingizi, na uchovu wa mara kwa mara.
3.Unapomsamehe mtu unapata faida nyingi zaidi kuliko anayesamehewa, kwani unapokaa na kisasi ni sawa na kukumbatia moto ukisubiri umchome mtu. Ukweli ni kwamba, utaendelea kuungua na kujiteketeza.
4.Hupunguza tatizo la shinikizo la juu la damu (High blood pressure)  na kiharusi. Unaposamehe, unaufanya moyo wako uende katika hali yake ya kawaida.
5.Hukusaidia kuwa huru zaidi. Ukisamehe mtu utahisi umeutua mzigo mzito sana hata kama mtu huyo hajakuomba msamaha.
6.Unapojaribu kulipa kisasi maana yake unachimba makaburi mawili, la adui yako na la kwako kwani Kisasi huwa hakimaliziki kwa kuwa daima hutarudhika, na adui daima ataona umemuumiza zaidi hivyo atahitaji kulipa kisasi pia. (eye to eye leaves the whole world blind) Jufunze Kusamehe ili maisha yaendelee.
7.Unaposamehe unakua kiimani, na itakuwa ngumu sana kwa mtu mwingine kukuumiza.
8.Huongeza siku zako za kuishi kwani usiposamehe utakosa furaha ya maisha. Utafiti unaonyesha kuwa watu wengi wenye umri zaidi ya miaka 70 wanauwezo mkubwa sana wa kusamehe, pengine ni moja ya sababu ya wao kuwa na maisha marefu zaidi.
9. Huongeza kujiamini na kuwa na mtazamo chanya (positive altitude)
10.Huimarisha mahusiano na kuongeza upendo kati ya ndugu, rafiki, au hata Mpenzi.
Kwanini Usisamehe leo? Hebu msamehe na share Somo hili na wenzako hapo chini. 
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system