Comments


HUYU HAPA MCHEZAJI BORA WA MEI VPL.

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu
ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom kwa mwezi Mei 2016.
Musa katika kinganyiro hicho aliwapiku Donald
Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo
Shooting. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi
tatu, Musa alicheza mechi zote tatu za timu
yake na kufunga jumla mabao manne; mawili
katika kila mechi.
Kwa kushinda tuzo hiyo ya Mei ambayo ni ya
mwisho kwa msimu huu kwa wachezaji bora wa
mwezi, Musa atazawadiwa kitita cha sh.
1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini
wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa
msimu huu wa 2015/2016 ambao mechi zake za
mwisho zilichezwa Mei 22 mwaka huu ni Hamisi
Kiiza wa Simba (Septemba), Elias Maguli wa
Stand United (Oktoba), Thaban Kamusoko wa
Yanga (Desemba), Shomari Kapombe wa Azam
(Januari), Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons
(Februari), Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar
(Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system