Golikipa David de Gea amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa 2015/2016 wa Manchester United kwa mara ya tatu mfululizo.
Baada ya De Gea kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo sasa amewashinda Roy Keane, Ruud van Nistelrooy na Cristiano Ronaldo ambapo kila mmoja aliichukua tuzo hiyo mara mbili ila yeye kafikisha tatu.
Aidha pamoja na kuchukua tuzo hiyo, mchezaji mwenzake Wayne Rooney ameonekana kuwa tofauti kwa kupewa tuzo hiyo De Gea kwa kuamini walistahili kuchukua wachezaji wengine.
“Kwa mimi binafsi, Daley (Blind) na Chris (Smalling) walikuwa bora zaidi kitu. Niliona Chris (Smalling) alifaa kuwa mchezaji bora kwa msimu uliopita na Daley (Blind) kwa msimu huu,” alisema Rooney.
Wengine waliochukua tuzo za mwaka ni Cameron Borthwick-Jackson kwa wachezaji wa chini ya miaka 21, Marcus Rashford mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wa miaka chini ya 18 na Anthony Martial akichukua tuzo ya goli bora la msimu alilofunga dhidi ya Liverpool.