Comments


WANAFUNZI 7000 WAREJESHWA NYUMBANI UDOM.

Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom)
kimewasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi
7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi
kwa ngazi ya stashahada na kuwataka
waondoke chuoni hapo mara moja.
tangazo lililotolewa jana chuoni hapo likiwataka
wanafunzi hao kuondoka kati ya jana hadi leo
saa 12 jioni. Tangazo hilo lilieleza kuwa
kutokana na matatizo yaliyopo katika
ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao
kurejea majumbani na wataelezwa mustakabali
wao “mapema iwezekanavyo”.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa
Kikula alipotakiwa kufafanua suala hilo, alisema
kwa ufupi kuwa suala hilo lipo lakini akaelekeza
apigiwe simu Ofisa Uhusiano wa chuo hicho,
Beatrice Baltazal kwa maelezo zaidi.
Baltazal alipotafutwa alisema kusimamishwa
kwa wanafunzi hao kulitokana na agizo la
Serikali na wametakiwa kulitekeleza.
Kuhusu lini na nini hatima ya wanafunzi hao,
alisema bado hawajui hadi hapo
watakapoelekezwa vinginevyo.
Hata hivyo, kulikuwa na malalamiko kwa
wanafunzi hao juu ya namna walivyopewa
taarifa za kusimamishwa masomo yao kwa
ghafla na kutakiwa kuondoka.
Kozi ya stashahada ya ualimu wa sayansi,
ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Jakaya
Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu
wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM pekee.
Waliokuwa na sifa za kujiunga na kupewa
mikopo ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne
na kufaulu vizuri masomo ya sayansi.
Wanafunzi hao waliokuwa wamekopeshwa na
Serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya
wenzao zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St.
Joseph kusimamishwa baada ya kubainika
hawakuwa na sifa za kudahiliwa.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system