Comments


POLISI WAZIDI KUUMIZA KICHWA MAUAJI YA DADA WA BILIONEA MSUYA.

Ikiwa bado kuna sintofahamu ya chanzo cha
mauaji ya dada yake bilionea Erasto Msuya,
Anneth, Polisi wamesema hawajabaini sababu
za awali za kifo hicho na wanaendelea na
msako wa waliohusika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles
Muroto alisema hadi jana wauaji walikuwa
hawajakamatwa, licha ya juhudi za upelelezi
zinazoendelea.
Tukio la Anneth Msuya aliyeuawa Alhamisi usiku
kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada,
Kigamboni jijini Dar es Salaam, limekuwa ni
mwendelezo wa matukio mengine ya uhalifu
kwa familia yao yaliyowahi kutokea baada ya
kifo cha kaka yake, Msuya.
Miongoni mwa wanaotafutwa na Polisi ni
mfanyakazi wa ndani aliyeondoka nyumbani kwa
Anneth mchana kabla ya kutokea mauaji hayo,
kwa madai kuwa hawezi kuendelea na kazi na
kuacha ufunguo kwa jirani.
Bilionea Msuya aliuawa Agosti 2012 kwa
kupigwa risasi, tukio lililofanyika mkoani
Kilimanjaro.
Ikiwa ni miaka minne tangu kifo hicho, kingine
kinatokea kwenye familia hiyo.
Dada wa Anneth, Ester, anayeishi Mbezi
Makonde jijini Dar es Salaam, alisema juzi kuwa
mazishi ya mdogo wake yatafanyika mkoani
Kilimanjaro Mei 30.
Bado watu wengi wanajiuliza kuhusu mfululizo
wa matukio katika familia ya Msuya, huku
wakishangaa sababu za binti huyo kuuawa
kama kaka yake.
“Ni kweli kifo hupangwa na Mungu, lakini siyo
kwa kifo hiki. Kwa nini wanauawa?” alihoji Juma
Majuto, mmoja wa waombolezaji wa msiba huo
uliopo Mbezi Makonde.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system