Comments


BAKWATA WAJA JUU WALAANI MAUAJI YALIYOTOKEA MSIKITINI MWANZA


Baraza Kuu la Waislam nchini Tanzania (Bakwata) limelaani vikali kitendo cha mauaji yaliyotokea kwa waumini watatu wa dini hiyo akiwa ni pamoja na Imamu wa msikiti ujulikanao kama Masjid Rahman wakiwa msikitini eneo la Ibanda Mkolani Jijini Mwanza yaliyotokea siku ya Mei 17 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Mufti Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi amesema kuwa kitendo hicho ni cha kinyama na ni kinyume na sheria za Tanzania hivyo Waislam na wananchi kwa ujumla wavipe ushirikiano vyombo vya usalama ili hatimaye wahalifu wa tukio hilo waweze kupatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa uharaka zaidi.

Aidha, Mufti Sheikh Zuberi ametoa maagizo kwa Bakwata Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu hali za majeruhi walionusurika katika tukio hilo ili waweze kupata nafuu na kurudi kushirikiana na familia zako.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system