Comments


Msimu wa 2015/16 Ligi ya Vodacom Tanzania Kutamatika hii leo kwa timu zote 16 kushuka katika viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu



Wakati ligi hiyo ikikamilika tayari klabu ya Yanga imesha tawazwa kuwa bingwa wa ligi hiyo na kukabidhiwa kombe lao Jumamosi iliyopita baada ya kufikisha pointi 72 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kati ya hizo zinazoshiriki ligi.

Wakati Yanga wakicheza mechi ya mwisho dhidi ya Majimaji bila presha kazi kubwa ipo kwa Azam na Simba ambazo zinapigania kumaliza nafasi ya pili baada ya kutofautiana kwa pointi moja Azam ikiwa kwenye nafasi ya pili na pointi 63 wakati Simba ikiwa ya tatu na alama zao 62.

Ushindani mwingine kwenye mechi za Jumapili ni kutafuta timu mbili zitakazo ungana na Coastal Union kushuka daraja baada ya timu hizo kuwa katika nafasi mbaya na endapo zitapoteza mechi zao za kukunja jamvi la Ligi Kuu huenda zikaipa mkono wa kwaheri ligi ya Vodacom, Timu hizo ni African Sports, Mgambo JKT zote za Tanga pia zipo JKT Ruvu, Toto Africans na Kagera Sugar.

Mechi nyingine za kufunga msimu leo zitakuwa kati ya mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu, Yanga itakayokuwa mgeni wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji wakati Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara.

Simba itakuwa uwanja wa taifa Dar es Salaam kucheza na JKT Ruvu, wakati Azam nayo itakuwa nyumbani Azam Complex kupambana na Mgambo JKT.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system