Comments


Mkapa amezitaka nchi za Jumuiya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhakikisha zinaendelea kusaidia nchi ya Burundi ili amani ipatikane.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Willium Mkapa, amesema kuwa hatma ya nchi ya Burundi ipo kwa wa Burundi wenyewe, hivyo amewashauri kukutana makundi yote yanayosigana ili wamalize tofauti zao. Aidha amezitaka nchi za Jumuiya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhakikisha nazo zinaendelea kusaidia nchi ya Burundi ili amani ipatikane.

Mkapa ameyasema hayo Jijini Arusha wakati alipokuwa akifungua kikao cha siku nne cha usuluhishi kwa makundi yanayopingana nchini Burundi kinachofanyika Arusha.

Amesema wenye jukumu la kuleta amani kwa nchi yao, ni Warundi wenyewe na kuwataka kukaa mezani moja ili kujadiliana pamoja na kuondoa tofauti zao kwa manufaa ya nchi yao.

Naye Balozi, Roeland Van der Geer akizungumza kwa niaba ya Jumuiya ya Kimataifa, amesema nchi ya Burundi inatakiwa kuhakikisha, amani inapatikana ili kuhakikisha kila raia wa nchi hiyo anapata maendeleo.

Balozi Geer ametoa rai kwa wananchi wa Burundi kuhakikisha mgogoro huo wa kisiasa unaisha na nchi inakuwa na amani.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system