Comments


DAKIKA 90 ZA KUAMUA KATI YA BATERN NA ATLETICO NANI KUTIMBA FAINALI

VIGOGO wa Germany Bayern Munich leo  Usiku wanatinga Uwanjani kwao Allianza Arena kurudiana na Atletico Madrid ya Spain katika Mechi ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huku wakitakiwa kupindua kipigo cha Bao 1-0 ili wao watinge Fainali.


Wiki iliyopita huko Vicente Calderon Jijini Madrid na Bao la Dakika ya 11 la  Niguez liliwapa Atletico ushindi wa 1-0.

Bayern wanatinga kwenye Mechi hii muhimu wakiwa na Majeruhi kadhaa ambao ni Holger Badstuber, Arjen Robben na Franck Ribery ambae huenda akarejea.

Atletico wao hawana Wachezaji majeruhi.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

Bayern Munich: Neuer; Lahm, Boateng, Martinez, Alaba; Muller, Vidal, Thiago; Costa, Lewandowski, Ribery

Atletico Madrid: Oblak; Juanfran, Godin, Gimenez, Luis; Saul, Gabi, Fernandez, Koke; F Torres, Griezmann

REFA: Cüneyt Çakır (Turkey)
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system