Fainali ya Kombe la FA kati ya Machester United na Crystal Palace imemalizika kwa Man United kuibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli ya Manchester United yakifungwa na Juan Mata dk. 81 na Jesse Lingard dk. 110 Huku goli pekee la Crystal Palace likifungwa na Jason Puncheon dk. 78
Kombe hilo limekuja katika kipindi kocha wa man United, Louis Van Gaal akiwa katika tetesi za kutimuliwa kazi kutokana na kushindwa kuiwezesha timu hiyo kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao hivyo kupatikana kwa ubigwa huo kunaonekana kuwa matumaini mema kwa kocha huyo na furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo iliyo na idadi kubwa ya mashabiki duniani kuliko vilabu vingine.
Aidha nahodha wa Man United, Wayne Rooney atakuwa ni moja wa wanafamilia wa Man United ambaye atakuwa na furaha zaidi kutokana na kuwa kombe la FA ndiyo kombe pekee ambalo alikuwa hajawahi kulishinda katika historia yake ya kucheza soka kwa upande wa vilabu na hivyo kushinda kombe hilo kwake inakuwa ni historia mpya ambayo alikuwa hajawahi ifikia.
Pamoja na ushindi huo pia Man United ilimaliza mchezo huo ikiwa pungufu baada mchezake wake Chris Smalling kumchezea faulo, Yannick Bolasie na kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Mark Clatternburg.
0 comments:
Post a Comment