Comments


VAN GAAL KUFUNGASHWA VIRAGO J3

Kwa mujibu wa BBC Manchester United wanataka kumtupia Louis van Gaal virago vyake Jumatatu kabla ya kumpa Jose Mourinho kibarua cha kuinoa klabu hiyo

Van Gaal ameiongoza United kutwaa Kombe la FA Jumamosi lakini dakika chache baada ya kunyanyua taji habari zilizuka kutoka kwa waandishi mbalimbali wa Uingereza kwamba muda wa Mdachi huyo klabuni umekaribia kufika kikomo.

BBC imeripoti kwamba Manchester United itamfukuza Van Gaal Jumatatu kabla ya kumtangaza Jose Mourinho baadaye wiki ijayo.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi van Gaal alionekana kujihami, "Nitawaonesha Kombe na sina muda wa kujadili (mustakaba wangu) na marafiki zangu wa vyombo vya habari ambao walinifukuzisha kazi tangu miezi sita iliyopita. Meneja gani anaweza kufanya nilichofanya?"

Van Gaal aliteuliwa kuwa kocha wa Manchester United 2014 baada ya kuachana na timu ya taifa ya Uholanzi aliyoiongoza kumaliza nafasi ya nne Kombe la Dunia, hata hivyo mashabiki wamezidi kuwa na hofu na mbinu za kocha huyo katika kampeni za Ligi Kuu Uingereza na kushindwa kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi kunaweza kumgharimu LVG kibarua chake.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system