Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo limetangaza kwa mara ya kwanza katibu mkuu mwanamke katika historia ya shirikisho hilo, FIFA imemtangaza Fatma Samba Diouf Samoura kutoka Senegal kuwa katibu mkuu wa kwanza wa shirikisho la hilo mwanamke.
Fatma Samba Diouf Samoura anaingia FIFA mwezi June kuanza kazi rasmi na kurithi nafasi ya Jerome Valcke katibu mkuu wa shirikisho hilo aliyefungiwa miaka 12 kutokujihusisha na soka, Samoura mwenye miaka 54 ametangazwa leo katika mkutano uliofanyika Mexico.
Rais wa sasa wa FIFA Gianni Infantino
FIFA imemtangaza Fatma Samba Diouf Samoura ambaye CV yake inaonesha kuwa amewahi kufanya kazi katika umoja wa mataifa UN
kwa miaka 21, mabadiliko hayo yamefanyika ikiwa ni muendelezo wa
mabadiliko katika shirikisho hilo, baada ya Rais wa zamani wa shirikisho
hilo Sepp Blatter kuachia ngazi.
0 comments:
Post a Comment