Comments


WALIO MUUA ASKARI WATIWA NGUVUNI

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema  Jeshi la Polisi linawashikilia watu 14 wanaosadikika kuhusika na kifo cha Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Ally Salum maarufu Kinyogori, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Mkuranga mkoani Pwani.

Taarifa iliyotolewa  na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi, imesema kuwa mauaji hayo yalifanyika juzi saa 1.30 jioni katika Kijiji cha Chatembo, Kata ya Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambapo watu wawili wakiwa wamevaa makoti meusi na kuficha sura zao, waliingia ndani ya uzio wa nyumba ya askari huyo wakiwa katika usafiri wa pikipiki aina ya Boxer.

Alisema katika tukio hilo, wauaji hao hawakuchukua kitu chochote zaidi ya ufunguo wa gari ambalo hata hivyo hawakulichukua ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali wa waliohusika na limeomba ushirikiano kutoka kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia wahusika kukamatwa kwa haraka.

Aidha Kamanda Sirro alisema tangu juzi Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi na oparesheni mbalimbali na kusisitiza “Waliofanya tukio hilo hata waende wapi watakamatwa tu, hili ni tukio la Mkoa wa Pwani lakini kwa sababu alikua anafanya kazi katika mkoa wangu taarifa hizo ninazo”.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system