Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Singida, Narumba Hanje, amewashauri viongozi wa
madhahebu ya dini mbalimbali kutenga muda wakati wa ibada kuliombea
taifa ili liweze kuondokana na mauaji ya kikatili ya watu wasio na hatia
yanayoendelea kushamiri hivi sasa kila kona ya nchi.
Hanje
ametoa wito huo juzi wakati akizungumza kwenye mazishi ya aliyekuwa
Afisa Mwandamizi wa Utafiti Kilimo Uyole Mbeya, Dk.Sofia Swai Mbogho,
yaliyofanyika katika kijiji cha Mtinko.
Hanje
ambaye amejibatiza jina la askofu wa kujitegema, alisema Tanzania hivi
sasa haina salama, imekubwa na balaa kubwa la watu wasio na hatia yoyote
kuuawa kikatili.
Akisisitiza,
alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa viongozi wetu wa madhehebu ya dini
wakatenga muda, kwanza kwa kuwakumbusha waumini wao kwamba kuuawa
binadamu mwenzake ni dhambi mbele ya Mungu.
“Pia
maombi au sala maalum zifanyike ili shetani ambaye amewaingia baadhi ya
Watanzania wenzetu kuanza kazi haramu ya kuuawa watu wasio na batia,
aweze kushindwa,” alisema Hanje.
Aidha,
mwenyekiti huyo amewaomba wananchi kutoa taarifa mapema Polisi endapo
watabaini dalili za viashiria vya viteno vya mauaji ya watu wasio na
hatia ili viweze kudhibitiwa.
Katika
hatua nyingine, Hanje amewataka viongozi wa dini wasijihusishe na
masuala ya uhaba wa sukari na kazi hiyo waiachie serikali ya awamu ya
tano ambayo tayari imeishachukua hatua la kumaliza tatizo hilo.
“Wafanyabiashara
wa sukari, nawaombeni mmuogope Mungu, acheni kuficha sukari …
mtawaomiza Watanzania wenzenu. Kadhalika acheni kuuza sukari kwa bei ya
juu, uzeni kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali yenu. Hii bidhaa ni
muhimu kwa maisha ya kila Mtanzania, muungeni mkono rais wetu kwa
kuhakikisha sukari inapatikana wakati wote, na kwa bei iliyotolewa na
serikali,” alisema.
Wakati
huo huo,Tamari Aron Mbogho (10), muda mfupi kabla ya kuagwa mama yake
Dk.Sofia, alimwimbia wimbo mama yake kwa kiingereza na kuutafsiri kwa
kishwahili,kitendo hicho kilipelekea baadhi ya viongozi wa dini na
waombolezaji kwa ujumla, kububujikwa machozi na wengi kushindwa kujizuia
na kulia kwa nguvu.
0 comments:
Post a Comment