Comments


Ronaldo uwezo alionao Rashford niwa kiwango cha juu.

Mshambuliaji chipukizi wa Manchester United, Marcus Rashford amezidi kupata umaarufu kutoka kwa wanamichezo wakubwa duniani pamoja na wadau wa michezo na kwa sasa amepata sifa kutoka kwa staa mwingine, Ronaldo.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil amesema kuwa uwezo wa Rashford ni mzuri kulinganisha na umri wake.
Ronaldo amesema uwezo alionao Rashford niwa kiwango cha juu na namuona kama mchezaji ambaye anaweza kuja kuchukua nafasi yake kwa kuwa na baadhi ya vitu ambavyo alikuwa akivifanya wakati wa enzi zake.
“Ni mchezaji mdogo lakini mwenye uwezo, ninaona baadhi ya vitu nilivyokuwanavyo vikiwa ndani yake, ni jasiri na anakuwa na kasi anapokuwa na mpira,
“Napenda washambuliaji ambao wana hasira na magori na hilo analo, naamini atakuwa na wakati mzuri katika maisha yake ya kucheza soka,” Ronaldo aliliambia gazeti la The Sun.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system