Comments


ACT KUWAPOKEA WALIOSIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE

Baada ya kutoka kwa taarifa kuwa
wabunge Zitto Kabwe na Halima Mdee
kuzuiliwa kuingia bungeni katika bunge la
bajeti, Chama cha ACT-Wazalendo
kimetoa taarifa kuhusu kusimamishwa kwa
wabunge hao ambapo mojawapo ni
Kiongozi Mkuu wa chama chao, Mh. Zitto
Kabwe.
Katika taarifa ambayo imetolewa na Katibu
wa Itikkadi, Uenezi na Mawasiliano, Ado
Sgaibu kupitia ukurasa wa Facebook wa
ACT amesema chama chao kimesikitishwa
kwa kitendo hicho lakini kwa upande
mwingine wanafarijika kwa kuona
wanafanyiwa hivyo kwa kuwatetea
wananchi.
“Chama cha ACT Wazalendo
kimesikitishwa na kitendo cha
ugandamizaji wa demokrasia
kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa
kuwasimamisha ubunge wabunge wa
upinzani akiwemo kiongozi wa chama
chetu ndg. Zitto Kabwe,
Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika
kuona wabunge hao wameondolewa kwa
sababu ya misimamo yao ya kutetea
maslahi ya wananchi, tungesikitishwa
zaidi kama mashujaa wetu hawa
wangeondolewa bungeni kwa sababu ya
ulevi au wawe sehemu ya wagonga mihuri
ya masuala ya hovyo hovyo
yanayosimamiwa na serikali ya chama cha
Mapinduzi (CCM),” ilisema taarifa hiyo.
Pia katika taarifa hiyo ACT wameeleza
kuwa wanaandaa maandamano
yatakayofanyika Dar es Salaam kwa ajili
ya kuwapokea wabunge ambao
wametolewa bungeni kwa sababu ya
kuwatetea wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM).
“Kwa sababu hiyo ya kusimamia maslahi
ya wananchi sisi kwetu ni mashujaa na
kwa maana hiyo Chama chetu kinaandaa
maandamano makubwa jijini Dar Es
Salaam kuwapokea mashujaa wa
wananchi,” ilieleza taarifa hiyo.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system