Wataalam wengi wa upasuaji wanafikiria wazo hilo ni la kiuwendawazimu, lakini sio kwa mtaalamu huyo, kwani anasema bado anapanga kujaribu pandikizo la kwanza la kichwa kwa binaadamu. (Head Transplant)
Dk. Canavero ambaye mpaka sasa ameshapata mtu wa kujitolea kufanya zoezi hilo, kijana mwenye asili ya Urusi ambaye ni mtaalam wa software Valery Spiridonov, ambaye ana tatizo la kupoteza nguvu kwa misuli yake ya mwili.
Dk. Canavero amesema mafanikio yake yameonesha kuwa mpango wake wa kupandikiza kichwa cha binadamu kwa mwili wa mtoaji (donor) bado upo, na ataanza mpango huo mwishoni mwa mwaka 2017 na unaweza kuwa njia ya kutibu waliopooza mwili.
“Ningesema tuna takwimu nyingi zinaendelea, ni muhimu kwa watu kuacha kufikiria jambo hili sio rahisi, hii inawezekana kabisa na tunaendelea kulifanyia kazi”, alisikika Dk, Canavero akimwambia mwanasayansi mchanga.
Timu iliyo nyuma ya kazi hiyo ilipost video ikimuonesha nyani ambaye alifanyiwa upandikizwaji huo, na kufanikiwa kutembea baada ya uti wa mgongo kutenganishwa na kuunganishwa tena'
Upandikizwaji wa kichwa kwa nyani ulifanywa katika chuo cha Harbin nchini China ( Harbin Medical University) na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, bila kuwa na muathiriko wowote katika uti wa mgongo, lakini aliuawa baada ya masaa 20 baadaye, kutokana na sheria za kazi.
Dk. Canavero amesema atahitaji pesa nyingi ili kuwalipa timu ya upasuaji, kwa mtu wa kwanza ambaye ni raia wa Urusi, hivyo amemuomba mwanasayansi tajiri zaidi Mark Zuckerberg, kufadhili upasuaji huo.
Picha ya Nyani aliyepandikizwa kichwa. |
Kijana Valery Spiridonov aliyejitolea kufanyiwa upandikizwaji huo wa kwanza, ambaye mwili wake una tatizo la misuli. |
0 comments:
Post a Comment