Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati),
akihutubia wakati wa uzinduzi wa duka na ghala la Bohari ya Dawa (MSD),
mkoani Mbeya leo hii. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean
Bwanakunu na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, Profesa Idrisa Mtulia.
Waziri Ummy akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka hilo.
Waziri
Ummy, akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu vibao
viwili kama ishara ya uzinduzi wa maghala ya mkoa wa Tabora na Tanga.
Waziri
Ummy (wa tatu kulia), akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya
Mbeya, Daud Msasi (kulia), jinsi Kanda hiyo inavyoandaa dawa na
kuzisambaza.
……………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
(mb), amezindua duka la dawa la MSD mkoani Mbeya na maghala matatu ya
kisasa ya kuhifadhia dawa yaliyopo mkoani Mbeya, Tanga na Tabora.
Waziri Mwalimu, ameipongeza MSD kwa kupata maghala matatu ya kisasa pamoja uanzishwaji wa duka la Mbeya.
Katika
hatua nyingine Waziri Mwalimu amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD vibao
viwili vya uzinduzi vinavyo wakilisha uzinduzi wa maghala ya Tanga na
Tabora.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema ghala na
duka lililofunguliwa litaiwezesha MSD kupanua uwezo wake wa kuhifadhi
dawa na vifaa tiba na pia kuongeza uwezo wa kusogeza huduma karibu na
wanachi.
Hata
hivyo, Bwanakunu ametoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa msaada wa
kiwanja cha hekari tano alioutoa kwa MSD. kiwanja hicho kipo eneo la
Luguruni na ambacho kitatumika kujengea ghala la kisasa la kuhifadhia
dawa kwa Kanda ya Dar-es-salaam.
Pia
amemuhakikishia Rais kwamba, pamoja na msaada huu wa kiwanja na kwakuwa
MSD inamahusiano mazuri na wadau wake wa maendeleo, kwasasa ipo kwenye
mazungumzo ili ujenzi wa ghala la Dar-es-salaam uanze mapema
iwezekanavyo na ikiwezekana mwezi Julai 2016. Kukamilika kwa ujezi huo
utapunguza kiasi kikubwa cha fedha kinacholipwa kila mwaka kama kodi ya
pango.
0 comments:
Post a Comment