Siku moja imepita toka michezo ya robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA ichezwe, usiku April 7 2016 michezo ya robo fainali ya Europa Ligi ambayo zamani ilikuwa ikifahamika kama UEFA ndogo ilichezwa pia katika viwanja kadhaa barani Ulaya.
Mchezo wa Borussia Dortmund dhidi ya Liverpool uliochezwa katika uwanja wa Signal Iduna Park Ujerumani ndio mchezo ambao ulikuwa na msisimko zadi usiku huo kutokana na kurejea kwa mara ya kwanza kwa Jurgen Klopp Signal Iduna Park kama kocha wa Liverpool na sio Borussia Dortmund.
Liverpool ya Jurgen Klopp ilimaliza mchezo huo kwa sare ya goli 1-1 baada ya Borussia Dortmund kusawazisha goli dakika ya 48 kupitia kwa Mats Hummels ikiwa ni dakika 12 zimepita toka Divock Origi aifungie goli Liverpool. Matokeo ya sare ni mazuri kwa Liverpool kwa Dortmund anatarajia kwenda Anfield kucheza robo fainali ya pili dhidi ya Liverpool April 14 2016.
0 comments:
Post a Comment