Usiku wa April 13 2016 ndio zilichezwa mechi mbili za mwisho za hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya, klabu ya FC Barcelona ilikuwa mgeni dhidi yaAtletico Madrid katika uwanja wa Vicente Calderon wakati FC Bayern Munichwalikuwa Ureno kucheza na Benfica.
FC Barcelona ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, wamevuliwa ubingwa kwa kufungwa jumla ya 2-0, hivyo kuondolewa mashindano kwa jumla ya goli 3-2, hiyo inatokana na matokeo ya mechi yao ya Nou Camp kuifungaAtletico goli 2-1.
Magoli ya Atletico alifunga Antoine Griezmann dakika ya 36 na dakika ya 88 akapachika goli la pili kwa mkwaju wa penati na kufanya nyota wa FC Barcelona kama Lionel Messina wengine kutoamini kilichotokea. FC Bayern wao wamepita kwa aggregate ya 3-2, baada ya mchezo wa leo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
0 comments:
Post a Comment