Kazi ipo! Video Queen asiyeishiwa vituko Bongo, Gift Stanford ‘Gigy
Money’ anadaiwa kuopoa kigogo ambaye ni mfanyabiashara wa madini, mkazi
wa jijini Arusha ambaye ndiye mwandani wake anayempa jeuri kwa sasa.
‘Ubuyu’ kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mwanadada
huyo unatonya kuwa, licha ya ‘umapepe’ wa Gigy ambaye kwa sasa safari za
Dar na Arusha hazikauki, ukweli ni kwamba jamaa huyo hapindui kwake.
Ili kupata mzani wa ubuyu huo, Over Ze Weekend lilimsaka Gigy,
alipopatikana kwa njia ya kilongalonga alikiri kuwa na kigogo huyo na
kudai kwamba wameshibana sana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment