Comments


TRUMP APIGWA CHINI NA TED CRUZ

Ted Cruz amshinda Trump mchujo Wisconsin


TrumpImage copyrightGetty
Image captionCruz ameshinda upande wa Republican, naye Sanders akashinda Democratic
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Ted Cruz ameshinda mchujo wa chama hicho katika jimbo la Wisconsin, hilo likiwa pigo kubwa kwa Donald Trump.
Katika chama cha Democratic, Bernie Sanders alipata ushindi mkubwa dhidi ya Hillary Clinton anayeongoza kwa wajumbe kwa sasa.
Bw Trump anaongoza kwa wajumbe na katika kura za maoni chama cha Republican, lakini kuna wasiwasi kwamba huenda akashindwa kupata wajumbe wa kumuwezesha kuidhinishwa moja kwa moja kuwa mgombea.
Wapinzani wa Bw Trump wanatumai kwamba hilo likifanyika basi wanaweza kubadilisha mambo katika mkutano mkuu wa chama hicho wa kuidhinisha wagombea mwezi Julai.
Katika mkutano huo, iwapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya nusu ya wajumbe, ni viongozi wa chama ambao watakuwa na usemi katika kuamua mgombea
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system