Comments


ROBOFAINALI UEFA KUTIMUA VUMBI KESHO

BARCELONA v ATLÉTICO MADRID
Bayern Munich v Benfica








Usiku  WA Mabingwa Watetezi wa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, FC Barcelona wako kwao Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain kucheza na wenzao wa Spain Atletico Madrid kwenye Mechi ya kwanza ya Robo Fainali
Mechi nyingine ya Robo Fainali Siku hiyo hiyo ni huko Munich, Germany wakati Bayern Munich watacheza na Benfica ya Portugal.
Barcelona wanaingia kwenye Mechi hii na Atletico Madrid wakitoka kwenye kipigo kitakatifu cha Jumamosi Uwanjani kwao Nou Camp mikononi mwa Mahasimu wao wakubwa Real Madrid waliowachapa 2-1 kwenye Mechi ya La Liga.
Kipigo hicho kilukuwa cha kwanza kwa Barca katika Mechi 39 chini ya Kocha Mkuu wao Luis Enrique.
Mbali ya hilo, Barca wanatinga kwenye Robo Fainali hii wakiwania kuwa Timu ya kwanza tangu Miaka ya 1990 kuweza kutetea vyema Taji lao la Ulaya ambalo wao walishindwa kufanya hivyo Mwaka 2010 na 2012.
Lakini Wachambuzi wengi, hasa wa huko Spain, wamekuwa na wasiwasi na Barca kwa sasa baada ya kuonekana wakiwa goigoi walipofungwa Juzi na Real.


-Barcelona wameshinda Mechi 6 zilizopita dhidi ya Atletico Madrid lakini katika Mechi yao pekee ya Ulaya, Atletico iliibwaga Barca kwa Jumla ya Bao 2-1 katika Mechi 2 za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Msimu wa 2013/14.

Lakini, Kocha Luis Enrique, mara baada ya kipigo toka kwa Real, amesema: “Tushaisahau Gemu hiyo!”
Ingawa Atletico hawana rekodi nzuri dhidi ya Barca, Timu hiyo ya Jiji la Madrid ni wapinzani wagumu na hasa kwa Mechi za Ulaya na Barca watakumbuka vyema nini walitendewa Msimu wa 2013/14 kwenye UCL.
Kwenye Hatua ya Robo Fainali ya UCL, kama hii, Barca walitoka 1-1 na Atletico Uwanjani Nou Camp na kunyukwa 1-0 huko Vicente Calderon na kutupwa nje ya UEAF CHAMPIONZ LIGI.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system