BONDIA Lulu Kayage yupo katika mazoezi mazito makali kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake wa kimataifa na Chiedza Homakoma ‘Nikita’ Malawi mpambano utakaofanyika mei 14 katika uwanja wa ndani
wa Taifa
Akizungumza wakati wa mazoezi yake anayofanya Kinondoni Msisiri amesema anajiandaa vizuri tu kwa ajili ya kumkabili mmalawi huyo atakaepigana nae aliongeza kwa kusema unajua rekodi yangu imeharibika kidogo kwa kuwa nilipigwa kwa pointi katika pambano langu la mwisho
Hivyo nimejipanga vizuri kuhakikisha nafanya vema katika mpambano huo wa kimataifa na ninawahidi mashabiki wagu kuwa siku hiyo nitakuwa radhi kufia ulingoni ili ushindi ubaki Tanzania na siwezi kupigwa hapa nchini nitatia aibu Taifa langu.
Siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi nchini
ambapo bondia Thomas Mashali atakumbana na Sajjad Mehrab kutoka ‘Irani’ ubingwa wa Dunia mkanda wa U.B.O
Mapambano mengine ya kimataifa yatawakutanisha bondia Ramadhan Shauri atakayepambana na Osgood Kayuni wa Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya huku Francis Miyeyusho akivaana na Frank Kiwalabye wa Uganda naye Nassibu Ramadhani atacheza na Edward Kakembo wa Uganda
Mapambano mengine ni kati ya Shaban Kaoneka atakayecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola
Mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga
siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi
0 comments:
Post a Comment