Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri klabu za
Azam FC na Young Africans ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika
michuano ya kimataifa itayochezwa wikiendi hii.
TFF imevitaka vilabu hivyo
kupambana katika michezo inayowakabili na kuweza kufanya vizuri kwa
kupata ushindi, ili kutengeneza mazingira mazuri katika michezo ya
marudaino itakayochezwa Aprili 19-20 mwaka huu.
Young Africans wanaochezwa hatua
ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afria (CAF CL) watashuka dimbani
kesho Jumamosi uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam saa 10 kamili kwa
saa za Afrika Mashariki, kucheza dhidi ya Al Ahly katika mchezo namba 89
wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL).
Mchezo huo utachezeshwa na Dennis
Dembele, akisaidiwa na Marius Donatien, Moussa Bayere, mwamuzi wa akiba
Tangba Kambou wote kutoka nchini Ivory Coast, huku kamisaa wa mchezo huo
akiwa Celestin Ntangungira kutoka nchini Rwanda.
Jumapili katika uwanja wa Azam
Complex uliopo Chamazi saa 9 kamili alasiri, Azam FC watwakua wenyeji wa
Esperance Sportive de Tunis (EST) ya Tunisa katika mchezo wa Kombe la
Shirikisho barani Afrika (CAF CC) hatua ya 16 bora.
Waamuzi wa mchezo huo namba 75 ni
Daniel Frazer Bennet, akisaidiwa na Zakhele Siwela, Thembisile
Theophilus, mwamuzi wa akiba Mbongiseni Fakudze wote kutoka nchini
Afrika Kusini, huku kamisaa wa mchezo akiwani Joseph Nkole kutoka nchini
Zambia.
0 comments:
Post a Comment