Comments


TCRA YAWAONYA WALE AMBAO HAWALIPI KODI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA limesema litachukua hatua kali za kisheria ikiwemo ya kutumia kampuni ya kudai madeni 1debt Collector1 kama njia mbadala kwa watoa huduma za mwasiliano watakaoshindwa kutimiza ahadi za kulipa madeni yao kwa mujibu wa makubaliano ya pande hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dr. Ally Simba ametoa onyo hilo wakati alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, akiwakumbusha watoa huduma ambao hadi sasa hawajalipa madeni yao kama walivyoahidi, hatua ambayo inakiuka sheria, kanuni na masharti ya leseni zao kwa kulipa ada na tozo wanazodaiwa.

Jumla ya watoa huduma kumi na wanane waliosimamishwa leseni zao ama kunyang’anywa wapo kwenye hatari ya kukumbwa na adhabu hiyo baada ya kushindwa kutimiza wajibu wa kulipa madeni yao kwa wakati na hata baada ya makubaliano.

Hata hivyo katika juhudi za kukusanya madeni hayo, katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 31 mwaka huu Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Bilioni 19.1.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system