Leo April 7, 2016 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 44 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi. Mzee Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964. Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya Muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Mzee Karume alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume
Hapa ndipo alipouwawa Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume miaka 44 iliyopita ndani ya ofisi za Makao Makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja, wakati akicheza bao na marafiki zake. Matundu yanayoonekana ukutani ni ya risasi ambayo muuaji alimimina kabla na yeye kuuwawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa Hayati Karume. Sehemu hii imewekwa uzio maalumu ili kupahifadhi kama kumbukumbu, kwani kila kitu kipo vile vile kilivyokuwa siku hiyoWanafunziwakitembelea mahali alipouwawa
0 comments:
Post a Comment