Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiongea na viongozi wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara Tanzania waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta jambo na viongozi wa
Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa
Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw. Johnsen Estomih Minja mara
baada ya kikao chao leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na
Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania leo jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. George Simbachawene amekutana na viongozi wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara Tanzania na kupata nafasi ya kusikiliza kero mbalimbali
zinazowakabili na kuahidi kushirikiana nao katika kutatua kero hizo.
Akizungumza na wafanyabiashara
hao waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi
wa Ofisi ya Rais-Tamisemi wamejadiliana masuala mbalimbali ya kibiashara
ili yaweze kunufaisha jamii na taifa.
“Nimesikia mapendekezo yenu
nitayafanyia kazi, nitawaita ili tujadiliane katika kujenga mazingira
bora na rafiki ya biashara yatakuwa na manufaa kwenu taifa kwa ujumla”
alisema Mhe. Simbachawene.
Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kwa dhati kushirikiana na wafanyabiashara nchini na
kulihakikishia taifa kuwa uchumi imara kulingana na Dira ya Maendeleo
ya Taifa ya mwaka 2025.
Katika kikao hicho
wafanyabiashara walipata nafasi ya kumueleza Mhe. Waziri kero mbalimbali
zinazowakabili zikiwepo utitiri wa kodi, ugumu katika upatikanaji wa
leseni na kukosekana kwa uwiano wa tozo za leseni kati ya sehemu moja na
nyingine ambapo Mhe. Waziri aliahidi kufanyia kazi kero na mapendekezo
mbalimbali ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara waliyowasilisha
kwake.
Akizungumza katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw. Johnsen
Estomih Minja alisema wafanyabiashara wanapenda kuona Tanzania ikikua
kiuchumi na wao kama wafanyabiashara wangependa kuwa wadau wa kuisaidia
nchi kukua kiuchumi, hivyo wanaomba serikali iweze kuwashirikisha katika
masuala mbalimbali yanayohusiana na masuala ya kibiashara ili waweze
kutoa mchango wao wa mawazo na kuondoa ugomvi kati ya wafanyabiashara na
Serikali yao.
Miongoni mwa masuala ambayo
Jumuia ya Wafanyabishara Tanzania imependekeza yaangaliwe kwa undani
kuwa ni pamoja na serikali kuangalia upanuzi wa wigo wa ulipaji wa
kodi,kuunganishwa kwa kodi na tozo mbalimbali katika ulipaji na
kurahisishwa kwa utaratibu wa ulipaji wa leseni.
0 comments:
Post a Comment