Comments


Lwakatare Ampinga Lowassa Kuhusu Wizi wa Kura.

Kwanza naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kuwasilisha taarifa hii kwani imepita takriban masaa 15 tangu nilipoona taarifa hii kwenye ITV Habari saa mbili usiku.Kwa hakika sikuamini kabisa nilipoona taarifa hii na nilijitahidi sana kusafisha mboni za macho yangu ili nione vizuri na kila nikiangalia hakika macho yalipatwa na ganzi.

Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred LWAKATARE akiongea mbele ya Makamanda wa CHADEMA kwenye Mji wa Kahama jana alisema kuwa anawashangaa baadhi ya viongozi wanaolalamika kuwa wanaibiwa kura wakati ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho. Anasema kuwa yeye anaongea kama Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA na amebaini kuwa Chama chake kimekuwa kikipoteza majimbo mengi kutokana na kukosa maandalizi ya kina. Alisema kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa ubunge jimbo la Bukoba Mjini baada ya maandalizi makubwa aliyofanya ya kuwaandaa vijana ambao watasaidia kumpa kura za kutosha. Ni kutokana na maandalizi hayo ndipo alipoibuka mshindi huku akimgaragaza mbunge mkongwe wa CCM, Dr HAMISI KAGASHEKI.

Kwa hali hiyo, aliwaasa CHADEMA na hasa kamanda LEMBELI kuanza maandalizi sasa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2020 badala ya kuhangaika Mahakamani ambako ni kupoteza muda na fedha. Naye Kamanda LEMBELI alisema kuwa, jimbo la Kahama lina Majipu mengi ambayo yanatakiwa kutumbuliwa. Alimuomba Rais Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza jimboni humo na yeye atahudhuria mkutano ambapo atakuwa na lengo moja tu la kumuonesha Rais Magufuli majipu yaliyojaa Kahama ambayo yanahitaji kutumbuliwa. Alisema kuwa Rais Magufuli ameanza vizuri na anaunga mkono utumbuaji majipu na kila mmoja anapaswa kumpa ushirikiano kwa vile ameonesha mwanzo mzuri.

MTAZAMO WANGU:

Ukitafakari kwa kina juu ya hoja za Lwakatare na Lembeli, utabaini mambo yafuatayo;

  • Kwa vile Lwakatare ni Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa CHADEMA, ni dhahiri kuwa chama hicho kinajua kuwa majimbo waliyoshinda, wameshinda kihalali na waliyopoteza ikiwa ni pamoja na Uchaguzi wa Rais wamepoteza kihalali.
  • Hoja za Lowasa kuwa aliibiwa kura hazina baraka ya chama hicho isipokuwa ni hoja zake binafsi 
  • Makamanda wengi wanamkubali Rais Magufuli na wanaunga mkono jitihada anazochukua. Ila wale Makamanda Maslahi ndio wanaoendelea kulalama wakiongozwa na Lowasa na Mbowe
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system