Comments


ZAO LA ALIZETI KUPEWA KIPAUMBELE


SERIKALI imesema itaweka mkakati katika uzalishaji wa alizeti ili kupunguza uingizwaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ambayo hugharimu Sh bilioni 500 kila mwaka.


Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba wakati alipofanya ziara wilayani Kondoa.
Alisema asilimia 80 ya mafuta ya kupikia yanaagizwa kutoka nje ya nchi na kugharimu Sh bilioni 500, fedha ambazo ni nyingi na lazima kuwe na mikakati ya kuongeza uzalishaji wa alizeti ili viwanda vya ndani vizalishe mafuta zaidi.


Pia aliwataka wananchi kuwa na tabia ya kulima mazao ya biashara kwa wingi kwani kwa kufanya hivyo watapunguza kuuza mazao ya chakula na kuwa na akiba ya kutosha.
“Msimu ujao mtengeneze mazingira ili kila mtu awe na ekari moja ya alizeti,” alisema.
Waziri huyo alisema serikali imejipanga kuhakikisha wakulima wanakuwa na masoko ya uhakika ya mazao wanayozalisha ya biashara.
Alitaka kutengeneza muundo wa ushirika ili bei ielekezwe kwenye masoko makubwa.


“Mkishafahamiana na makadirio ya mavuno ili pale unapoongelea soko unajua Kondoa kuna kiasi gani cha ufuta.”
Pia alisema wizara hiyo inaandaa utaratibu wa matumizi ya ardhi kwa wafugaji wenye mifugo kuanzia 1,000. Alisema kwa upande wa makundi wa wafugaji wadogo kuna mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system