Hakuna jambo jipya duniani ila nikuongezea tu ama kuboresha vilivyokuwepo ndio maana aliyetengeneza Ulimwengu huu amekaa kando anatazama kila tunalofanya na maisha yanasogea tena kwa kasi ili kutoa nafasi kwa watu kuboresha vile vya zamani.
Kwenye ulimwengu wa soka uliochini ya mamlaka ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao ni kama Adolf Hitra na Benito Mussolini, kila mchezaji anajaribu kufanya kila awezalo ili angalau siku moja aweze kuwekwa kundi moja na hawa jamaa wawili.
Ushindani wa mafanikio usio na kikomo ndio unazalisha mabao kama hakuna magolikipa kwenye ligi ya La liga. Jana safu inayotajwa kuwa ndio safu hatari zaidi ya ushambuliaji kuwahi kutoka “MSN” wakiwa ugenini walitoa onesho kali baada ya kupotea kwenye gemu kwa takribani wiki mbili wakaitandika Deportivo la coruna magoli 8 – 0 Suarez akiingia kambani mara 4 na kufikisha alama 79 sawa na Atletico Madrid.
Historia inasemaje?
Suarez kwasasa amefikisha jumla ya mabao 47 msimu huu kitu ambacho kimewahi kufanywa miaka kumi iliyopita yaani msimu wa 1996 chini ya fundi na nguli wa kuzifumania nyavu duniani Ronaldo LuÃs Nazário de Lima akikipiga palepale Barcelona. Ama kweli duniani hakuna jipya.
0 comments:
Post a Comment