Comments


KLOPP ALAMBA MKATABA MPYA NA LIVERPOOL


Licha ya kutokushinda taji lolote kwa msimu wa 2015/2016 lakini bado hilo halijawa kigezo cha wamilikiwa klabu ya Liverpool kukataa kuendelea kufanya kazi na kocha wa klabu hiyo, Jurgen Klopp.

Liverpool imetoa taarifa kuwa imemuongezea mkataba mrefu zaidi wa miaka sita kocha wake, Klopp ili aendelee kuinoa klabu hiyo mpaka mwaka 2022 maamuzi ambayo yamekuja baada ya kuibadilisha Liverpool kwa kiasi fulani japo haikwataa taji lolote lakini ilifanikiwa kufika hatua ya fainali ya Uefa Europa.
Pamoja na Klopp kuongezewa mkataba, pia makocha wasaidizi wa mjerumani huyo, Zeljko Buvac na Peter Krawietz nao wameongezea mkataba sawa na mkuu wao wa kazi, Klopp.
Taarifa ya Liverpool inaeleza kuwa uamuzi wa kumuongezea Klopp mkataba ulikuja siku ya Jumatano ambapo wamiliki wa klabu, Fenway Sports Group (FSG) walitaka kuendelea kufanya kazi na Klopp kwa miaka mingi na ndipo walipofanya nae mazungumzo na baada ya kukubaliana amesaini mkataba mwingine.
Akizungumza na mtandao wa Liverpool, Klopp amesema “Ni ngumu kuelezea kwa maneno jinsi ambavyo ninajisikia mimi, Zeljko na Peter kwa jinsi tumevyokubalika kwa wamiliki wa timu na kwa klabu kwa ujumla”

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system