Ndege ya kubeba abiria ya Shirika la Batik Air
Jakarta – Indonesia
UWANJA wa Ndege wa Mji wa Jakarta nchini Indonesia umefungwa kwa muda baada ya ndege mbili kugongana usiku wa kuamkia leo.
Ndege ya kubeba abiria ya Shirika la Batik Air ambayo ni Air Boeing 737-800, yenye namba za usajili PK-LBS na namba ya safari 7703 kutoka Jakarta Halim Perdanakusuma kwenda Ujung Padang (Indonesia) ikiwa na abiria 49 na stafu 7 wakati ikipaa, ubawa wake uligonga sehemu ya nyuma ya ndege ya Shirika la TransNusa yenye namba za usajili PK-TNJ iliyokuwa ikibururwa kwenye njia ya kutumiwa na ndege kupaa au kutua.
Ndege ya kubeba abiria ya Shirika la Batik Air iliyopata ajali.
Ubawa wa pembeni wa ndege ya Batik Air uligonga mabawa ya nyuma ya ndege ya TransNusa na bawa la kushoto na kusababisha tenki la mafuta la ndege ya TansNusa kupasuka na kushika moto papo hapo.
Muda mfupi tu kikosi cha zimamoto cha uwanjani hapo kilifika eneo la tukio na kuanikisha kuuzima moto huo.
Hata hivyo abiria na stafu wote walifanikiwa kuokolewa salama, Maafisa wa Usalama nchini humo wanasema hakuna aliyejeruhiwa wakati wa ajali hiyo.
Kisa hicho kilitokea katika uwanja wa ndege wa Halim Perdanakusuma mjini Jakarta ambao sana hutumiwa kwa safari za ndege za ndani ya nchi.
Ndege ya Shirika la TransNusa iliyopata ajali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, ndege hiyo ya Batik Air ilikuwa na watu 49, abiria pamoja na marubani.
Msemaji wa kampuni ya Lion Air Group, inayomiliki Batik Air ameambia mashirika ya habari ya kimataifa kwamba rubani amekatiza safari baada ya ajali hiyo na abiria wako salama.
Maafisa wa wizara ya uchukuzi ya Indonesia wamesema ndege hizo ziliharibiwa wakati wa kisa hicho. Video iliyopakiwa mtandaoni inaonesha miali ya moto ikitoka kwenye ubawa wa ndege ya Batik Air.
Indonesia ina historia mbaya ya usalama wa ndege licha ya kuendelea kufana na uchukuzi wa ndege hasa ndege za kubeba abiria za bei nafuu.
Ramani kuonesha eneo la tukio ambapo ndege hizo zimegongana.
Mwaka 2013, ndege ya Lion Air ilipita njia ya uwanja wa ndege wa Denpasar, Bali na kutumbukia baharini. Watu 22 walijeruhiwa.
Mwaka uo huo, ndege nyingine ya Lion Air iliteleza ikitua kisiwa cha Sulawesi na kugonga ng’ombe.
Mwaka 2014, ndege ya kampuni ya AirAsia nchini Indonesia iliyokuwa safarini kutoka Surabaya hadi Singapore ilianguka baharini na kuua watu wote 162 waliokuwa ndani.
0 comments:
Post a Comment