Shirikisho la Soka Zanzibar limekuwa na migogoro kipindi kirefu baina ya viongozi wenyewe na kupelekea maswala ya soka kuhamia mahakamani

GOAL

Baada ya mgogoro wa muda mrefu, hatimaye chama cha soka Zanzibar kimepata Rais wake mpya, Bw. Ravia Idarous Faina kuliongoza shirikisho hilo.

Huu ni muda muafaka kwa Ndugu Ravia na viongozi wenzake kuwarejeshea Wazanzibari hadhi ya soka lao, jukumu kubwa likiwa kutafuta wadhamini wa Ligi Kuu ya Zanzibar ambayo imekosa mvuto. Wadhamini watakaorejesha motisha kwa klabu, wachezaji na mashabiki hali kadhalika ili kuongeza ushindani wa ligi hiyo.
Kipindi shauri la ZFA lilipokuwa mahakamani, TFF chini ya Jamal Malinzi lilijaribu kutatua migogoro hiyo ya Zanzibar bila mafanikio hali iliyopelekea kuwa na mvutano baina ya mashirikisho hayo mawili.

Baada ya kupatikana rais mpya, Ravia anayeonekana kuwa na ushawishi mkubwa moja ya jukumu lake jingine ni kurejesha umoja na uhusiano chanya baina ya ZFA na TFF ili kwa pamoja waweze kukuza soka la Tanzania.
Viongozi wapya wa ZFA wanatakiwa kurudisha mashindano yaliyo potea kwa hivi karibuni kama ligi ndogo, Kombe la Muungano, mashindano yaliyozipa timu za Zanzibar umaarufu na ubora miaka ya 2000, mfano mzuri ukiwa ni KMKM.
Kwa miaka mingi sasa Zanzibar wamekuwa wanachama wa CAF, wamejitaidi sana kupata uanachama FIFA bila kuwa na mafanikio yeyote. Muda wa Bw. Ravia Idarous na uongozi wake kujenga historia yao na kuacha alama kwa kuisaidia Zanzibar kuingia kwenye uanachama wa FIFA nido huu.