Comments


MARUFUKU MAGARI YENYE UZITO KUPITA KATIKA DARAJA LA NYERERE

Hivi ndivyo mandhari nzuri na ya kuvutia ya Daraja la Nyerere lionekanavyo kwa juu pamoja na flai ova yetu ya kuingilia darajani hapo ndani ya Wilaya mpya ya Kigamboni.
Sehemu ya mageti ambapo magari yanapaswa kupita wakati wa kufanya malipo yanayotarajiwa kuanza Mei Mosi 2016.
Mhandisi wa Mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) Jamal Mruma akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari kuhusiana na ubora wa daraja hilo.Mhandisi Mruma alisema kuwa Daraja hilo limejengwa kwa ubora mkubwa na lina uwezo wa kuhimili uzito zaidi ya tani 50,lakini kwa sasa magari yanayoruhusiwa ni yale yenye tani kumi kushuka chini,”kwa sasa tunadhibiti uzito mkubwa kwa sababu kuna baadhi ya maeneo bado hayajakamilika ikiwemo na barabara ya kuingilia Kigamboni,ambako hakuwezi kumudu kupitishwa uzito mkubwa”,alibainisha Mhandisi Jamal.
Meneja Mradi kutoka NSSF,Mhandisi Karim Mataka akizungumzia namna baadhi ya Madereva ambao wamekuwa wakikiuka taratibu/sheria na alama zilizowekwa katika daraja hilo kubwa Afrika Mashariki ambalo linatarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 100 iwapo litapata matunzo stahiki.
Mhandisi Karimu amebainisha kuwa magari yanayopaswa kupita hapo kwa sasa yawe chini ya tani 10,kwa sababu kwa upande wa Kigamboni bado baadhi ya barabara hazijakamili,hivyo ni vyema Madereva wote wakawa makini.
 
Daraja hilo ambalo litaanza kutumika rasmi kwa kulipia Mei Mosi 2016,Mhandisi Karimu amewataka Watanzania kulinda miundo mbinu ya daraja hilo ikiwemo kutii sheria zote za Daraja hilo ili kuepuka kusababisha uharibifu wa aina yoyote ile,kwa sababu limejengwa kwa gharama kubwa na linahitaji matunzo.

Mhandisi alibainisha pia kuwa Daraja hilo la Kigamboni ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na kulibatiza jina la Daraja la Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Moja ya Lori likikatiza darajani hapo kwa kukiuka taratibu na sheria za Daraja hilo.
DCIM100MEDIADJI_0006.JPG
Muonekano wa Daraja la Mwal Nyerere kama lionekanavyo kwa mbaali kidogo unapoelekea kwenye mageti ya kutokea upande wa pili wa Kigamboni.Daraja hilo limerahisisha usafiri wa kutoka Kigamboni mpaka kati kati ya jiji la Dar.
DCIM100MEDIADJI_0011.JPG
CgMM5g4UAAA8hhP
Daraja la Kigamboni linavyoonekana usiku.
DCIM100MEDIADJI_0053.JPG
Daraja la Kigamboni linavyoonekana mchana.
DCIM100MEDIADJI_0060.JPG
Makutano ya barabara za kutoka na kuingia katika daraja la Kigamboni yanavyoonekana.

DCIM100MEDIADJI_0069.JPG
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system