Comments


OBAMA ASIKITISHWA NA MAUAJI ORLANDO

Rais wa Marekani,Barack Obama amesema
shambulio la risasi katika Klabu ya usiku mjini
Orlando ni la kigaidi na ni kitendo cha chuki
Takriban watu 50 wamepoteza maisha na
wengine 53 wamejeruhiwa siku ya Jumapili,
baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha
kufyatulia risasi Klabu moja ya usiku iliyokuwa
ikiwakutanisha watu wa mapenzi ya jinsia moja
mjini Orlando nchini Marekani.
Polisi nchini humo wamesema kuwa ni shambulio
baya kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Rais Obama amesema Marekani inaungana ikiwa
na huzuni,mshtuko mkubwa na inalenga kutetea
watu wake, pia amesema mauaji hayo
yanawakumbusha ni namna gani ilivyo rahisi
kupata silaha hatari nchini Marekani.
Shirika la kijasusi nchini humo,FBI limemtambua
mshambuliaji huyo kuwa raia wa Marekani,Omar
Mateen ambaye naye aliuawa wakati wa
mapambano na vikosi vya usalama katika klabu
hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya watu 300 ndani
yake.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system