Tangu Nay wa Mitego aachane na Shamsa Ford, bado hajamuonesha mrembo mwingine aliyeuhamishia moyo wake.
Na sasa huenda amempata yule anayeweza kuanza kuwaonesha mashabiki. Rapper huyo wa ‘Shika Adabu Yako’ amepost kwenye Instagram picha ya msichana mrembo mwenye asili ya Kisomali na kuashiria kuwa tayari ameshampata mrithi wa ex wake.
Na hivi karibuni Nay ambaye amejitolea kumsaidia mzazi mwenzake, Zuwena aliyefungwa jela miaka miwili kwa kosa la kutishia kusambaza picha za utupu za mpenzi wake, aliiambia Bongo5 kuwa tayari ana mpenzi mwingine.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment