Louis van Gaal hana mpango wa kuendelea kubaki
Manchester United baada ya msimu huu na amekataa kujadili swala hilo na
vyombo vya habari
Ushindi wa 2-1 wa Manchester United dhidi ya Everton katika uwanja wa
Wembley uliwapatia Mashetani Wekundu tiketi ya kutinga nusu fainali ya
Kombe la FA na fursa kubwa zaidi kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza
tangu 2004, hali kadhalika kumpunguzia presha kocha van Gaal.Kwa kiasi kikubwa inatarajiwa Mdachi huyo ataondoka United majira ya joto licha ya kuwa na mwaka mmoja zaidi katika mkataba wake lakini hayupo tayari kujadili jambo lolote nje ya bodi ya United.
Alipoulizwa jinsi gani ushindi dhidi ya Everton unampa tumaini kuelekea msimu ujao, van Gaal alisema: “Sina mpango wa kuendelea zaidi ya msimu huu.”
Lakini alikataa kueleza matamshi yake kwa undani: “Tunaishi kwa wakati uliopo, kwa habari ya baadaye nitajadili na bodi yangu ya wakurugenzi na si wewe.”
Kwa mtazamo wa haraka ni jambo lisiloepukika van Gaal kuenguliwa Old Trafford mwisho wa msimu huu na huenda hilo lisibadilike hata kama United wakitwaa kombe la FA ambalo wamelikosa tangu 2004.
Lakini swali la msingi, Je! United ikitwaa kombe la FA na kufanikiwa kutinga nne bora Ligi Kuu ya Uingereza, hiyo itatosha kumpa van Gaal nafasi ya kubaki Old Trafford hadi mkataba wake utakapokoma mwakani?
0 comments:
Post a Comment