Comments


MBARAWA >>>Sito vumilia watendaji wazembe na wasiotaka kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano.

Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa wizara yake haitawavumulia watendaji wazembe na wasiotaka kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano.


Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo alipotembealea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa nchiniTanzania (TMA) na kubainisha kuwa anawataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu na kuwatendea haki watanzania ambao kwa kiasi kikubwa wanawategemea wao kujua masuala mbalimbali yahusuyo hali ya hewa.mbarawa


Aidha, Profesa Mbarawa amesema kuwa anaitaka mamlaka hiyo kuanzisha utaratibu wa kupima utendaji kazi wa wafanyakazi kwa mwaka mzima ambapo ndio kitakuwa kigezo cha kumpandisha daraja mfanyakazi au kumuongezea mshahara.

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa ameitaka mamlaka ya hali ya hewa nchini kuachana na mfumo wa zamani wa kuhifadhi kumbukumbu zao kwa njia ya makaratasi na badala yake watumie njia ya komputa njia ambayo ni rahisi na inabana matumizi ya karat
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system