RAPA maareufu duniani, Tyga ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia uhusiano wa kimapenzi kati ya aliyekuwa mpenzi wake, Blac Chyna na Rob Kardashian ambaye ni mdogo wake Kim Kardashian baada ya wawili hao kukaririwa hivi karibuni wakijianika kuwa ‘wanadate.’
Tyga na Blac Chyna ni wazazi wa mtoto aitwaye King Cairo na waliachana hivi karibuni.
“Kila mtu ana haki ya kuwa na furaha. Kile mtu anafanya kwa ajili ya furaha yake hakinihusu, ilihali hakivurugi furaha yangu,” Tyga alisema kupitia Twitter.
“Inanipa faraja kuona mama wa mtoto wangu akiwa na furaha. Kinachonipa shida kwenye hili ni kuhusu mwanangu (King Cairo). Ninahitaji awe mwenye furaha.”
Penzi la Chyna na Rob lilizua gumzo mitandao baada ya kuleta sintofahamu ndani ya familia ya Kardashian kwani Tyga naye kwa sasa anauhusiano wa kimapenzi na mdogo wake Rob Kardashian aitwaye, Kylie Jenner.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment